Unafahamu nini kuhusu Kuku wa Nyama (Broiler)
Broiler ni jamii ya kuku wafugwao mahususi kwa ajili ya nyama. Faida nyingine ni mifupa yake kutumika kama chakula cha mifugo mingine, kinyesi chake kutumika kama mbolea ya mazao n.k.
Aina kuu za Broiler wafugwao Tanzania kwa sasa;
1.Cobb 500
2. Ross 308
3. Arbor Acre plus
4. Hubbard efficiency plus
Aina hizi za broiler zina ukuaji unao tofautiana hivyo nakushauri kabla huja weka order hakikisha unajua aina ya kuku unao taka kufuga mfano, ona uzito wa kuku kwa siku ya 21.
1.Cobb 500 uzito wa 1.116kg chakula alichokula ni 1320
2. Ross 308 uzito wa 0.929kg chakula alichokula ni 1.180kg
3. Arbor Acre plus uzito wa 1.006kg chakula alichokula ni 1.163kg
4. Hubbard efficiency plus, uzito wa 1.008kg chakula alichokula ni 1.19
Katika mradi wa ufugaji wa Broiler 70% ya jumla ya gharama za mradi ya Chakula. Hivyo hakikisha kuku anakula chakula bora na kwa kiwango chake, pia hakikisha chakula hakimwagiki bandani kuepusha upotevu wa chakula na pia
Madaraja ya vyakula vya Broiler
Broiler starter crumble/mash
Broiler grower pellet/mash
Broiler finisher pellet/mash
Ili kupata matokeo mazuri katika mradi wako tumia crumble au pellet (vyakula vya punje).
FANYA HAYA ILI KUKU WAKO WAENDELEE KUTAGE MAYAI MENGI.
1. Wape chakula bora chenye virutubisho vya kutosha pamoja na maji safi na salama. Usijaribu kuchakachua au kuwapunguzia chakula chao hawatataga na hawatakupa matokeo mazuri.
2. Viota vyao viwe safi. Safisha viota vyao mara kwa mara ili watage sehemu safi. Hakikisha pia viota vyao vina giza kiasi, usiruhusu kuku au mayai kuonekana kwa urahisi.
3. Wawe na sehemu ya wazi ya kuzunguka zunguka na kupanda juu kama kuwa na vichanja au bembea.
4. Wawekee calcium ya kutosha kwenye chakula chao ili mayai wanayotaga yawe na gamba gumu.
5. Wachunguze mara kwa mara kama wana dalili za kuumwa, na endapo dalili zipo watibu mara moja.
6. Wapatie maji safi kila siku. Pia safisha vyombo vyao kwa sabuni kila siku.
7. Hakikisha banda lao ni safi muda wote ili kusiwe na wadudu kama viroboto, chawa na papasi. Wadudu hawa huwasumbua kuku na kuwafanya wapunguze kutaga.
8. Hakikisha kuku hawapati msongo/stress, mfano kusiwe na wanyama wa kuwatisha wanaopita au kuingia bandani kwao.
9. Chagua aina sahihi ya kuku wanaotaga mayai mengi.
10. Umri wa kuku. Kuku wenye umri wa miezi 6 - 18 wanataga sana. Wakiwa na miezi 19 - 24 wananyonyoka manyoya (Annual Molt), hivyo hupunguza kutaga, na wakianza kutaga tena, wanataga mayai makubwa na machache kuliko mwanzo.
11. Wasihamishwe hamishwe banda. Kuku hutaga vizuri zaidi wakiwa kwenye mazingira waliyoyazoea.
Kuna aina nyingi za kuku wa mayai (Layers) lakini kwa aina hii ya kuku Bovan Brown, ni moja ya kuku mwenye sifa nyingi sana ikiwemo kuku mmoja anauwezo wa kutaga Mayai 320 hadi 350 Ndani ya miezi 12.
Kuku huyu anauwezo wa kutaga kwa muda wa miezi 18 mfululizo kabla ya kuacha kutaga.
Anaanza kutaga akiwa na umri wa wiki 18 (miezi 4 na siku 14) hadi wiki 20 (miezi 5)
SIFA ZA HAWA KUKU (BOVANS BROWN)
Wanakuwa vizuri sana
Wanataga wakishafika miezi 5 toka akiwa kifaranga.
Wanastahimili magonjwa.
Utagaji wao asilimia 95
Wanataga mayai mpaka 250+ kwa mwaka.
Wanakaa miaka 2 ukiwatunza vizuri.
Banda bora la kuku wa mayai, nyama au chotara lina nafasi kubwa ya kuamua afya, uzalishaji na faida ya ufugaji wako. Ili banda liwe bora, lazima uzingatie mambo yafuatayo:
1. Mahali na Mwelekeo wa Banda
Mahali: Pawe sehemu kavu, pasipo na mafuriko, palipo mbali na kelele na wanyama wakali.
Mwelekeo: Banda lipangwe mashariki – magharibi ili jua lisipige moja kwa moja muda wote, na kuhakikisha hewa inatembea vizuri.
2. Ventilation (Uingizaji Hewa)
Banda liwe na madirisha au matundu ya hewa pande mbili kwa urefu mzima, yakifunikwa na wavu wa chuma au neti dhidi ya ndege wadogo na wadudu.
Uingizaji hewa mzuri hupunguza harufu, unyevunyevu na magonjwa.
3. Sakafu
Sakafu ya zege ni bora kwa urahisi wa kusafisha na kuzuia wadudu kama chawa na funza.
Ikiwa ni deep litter system: weka majivu, kisha randa za mbao ndogo ndogo (wood shavings), pumba za mchele au nyasi kavu juu ya zege.
Ikiwa ni cage system: hakikisha kuna mfumo wa kukusanya kinyesi chini.
4. Ukuta na Dari
Ukuta unaweza kuweka kozi moja ya tofali kwa sehemu zenye joto kama Dar na Mwani ila kwa sehemu ambazo zina baridi unaweza kuweka hata kozi tatu (3) za tofali.
Dari (paa) liwe na urefu wa angalau mita 8 au 12 centimeter ili kuruhusu hewa kupita vizuri.
Paa lipauzwe vizuri kuzuia joto kali na mvua.
5. Vifaa vya Ndani
Vyombo vya maji (drinkers), zisambazwe vizuri, kila kuku 50–75 wawe na access ya drinker moja.
Vyombo vya vyakula (feeders): zisambazwe sawasawa ili kuepuka msongamano.
Viota vya kutagia (nesting boxes): kama ni floor system, weka kikapu au box moja kwa kuku 5–6.
Ikiwa ni cage system, box za kutagia hujengwa moja kwa moja kwenye cage.
6. Mwanga
Kuku wa mayai wanahitaji masaa 16 ya mwanga kila siku ili watage vizuri.
Weka taa za umeme ndani ya banda (bulb za kawaida au energy saving).
7. Usalama
Banda lifungwe vizuri kuepusha wanyama wakali, wezi na ndege waharibifu.
Eneo la banda liwe na uzio.
8. Huduma ya Maji na Umeme
Maji safi ya bomba au kisima karibu.
Umeme wa taa na kifaa cha dharura (generator au solar) kama umeme ukikatikakatika.
9. Usafi na Afya
Lete mfumo rahisi wa kusafisha kinyesi.
Tenga sehemu ndogo ya isolation (karantini) kwa kuku wagonjwa.
NB: Kwa kifupi, banda bora linatakiwa:
Liwe safi, kavu, lenye hewa ya kutosha, taa, sehemu ya maji na chakula, sehemu ya kutagia, na liwe salama.